USAWIRI WA WAANDISHI WA JINSIA TOFAUTI WANAVYOANGAZIA UKANDAMIZAJI WA KIJAMII KATIKA RIWAYA ZA MAISHA KITENDAWILI NA CHOZI LA HERI

AINA MBALIMBALI ZA UKANDAMIZAJI WA KINJINSIA KWA MUJIBU WA CHOZI LA HERI NA MAISHA KITENDAWILI

  • Jackline Njeri Murimi
  • Maingi Nkoroi Nancy
Keywords: Jinsia, ukandamizaji, Kijamii .

Abstract

IKISIRI

Katika utafiti huu tumehakiki jinsi waandishi wa kiume na kike wanavyoangazia ukandamizaji wa kijinsia katika jamii kwa kurejelea riwaya za Chozi la Heri (Assumpta K. Matei) na Maisha Kitendawili (John Habwe).  Utafiti huu unachunguza na kuchanganua kwa misingi ya kijinsia jinsi wahusika mbalimbali wanavyotengwa na kukandamizwa na jamii. Aidha, utafiti umechanganua jinsi waliotengwa na kukandamizwa na jamii wanavyosawiriwa katika macho ya waandishi wa kiume na wa kike. Isitoshe mapendekezo ya utatuzi wa matatizo haya yamedokezwa kwa kurejelea waandishi John Habwe na Assumpta K. Matei. Imebainika kuwa John Habwe amesawiri jinsia ya kike kama jinsia inayokandamizwa zaidi mikononi mwa yule wa kiume tofauti na Assumpta Matei ambaye ameangazia jinsia ya kiume kama jinsia iliyo na matatizo mengi ikilinganishwa na ile ya kike. Utafiti huu, uliongozwa na nadharia ya Jinsia - Hakiki iliyoasisiwa na mfeministi Showalter Elaine katika mwaka wa 1840. Nadharia hii hutumiwa kuhakiki kazi za kifasihi zilizoandikwa na watunzi wa jinsia tofauti tofauti. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu mathalan utafiti wa maktabani ambapo tulisoma vitabu, majarida, matini na magazeti mbalimbali ili kukusanya data yetu. Pia tumesoma maandishi mbalimbali yanayolenga mada yetu hasa yale yaliyoandikwa na jinsia ya kiume na kike kuhusu ukandamizaji. Zaidi ya hayo, tumechakura mtandao ili kuweza kuelewa zaidi kuhusu kipengele cha ukandamizaji katika jamii. Tumetumia uteuzi wa sampuli wa kiamksudi katika kuteua riwaya ya Maisha Kitendawili na Chozi la Heri. Riwaya hizi mbili zimeandikwa na watunzi mwanamume na mwanamke ambao ni watunzi wa kazi za Kiswahili nchini Kenya. Tulikusanya data yetu kutoka kwa riwaya ya Maisha Kitendawili na Chozi la Heri.  Aidha, tulipata data yetu kutoka mtandaoni, vitabuni, makala, maktabani na kwenye tasnifu. Tuliichanganua data yetu kwa kutumia maelezo na tarakimu, maelezo na ufafanuzi kuwasilisha data. Data hii ilitusaidia kutathmini kama waandishi wa jinsia ya kiume na kike wanaangazia masuala ya ukandamizaji kwa njia sawa ama kwa njia tofauti.

Utafiti huu unanuiwa kunamfaa mwanafasihi katika kupata maarifa na uzoefu wa uhakiki kuhusu mwanajamii aliyetengwa na kuelewa kwa undani kazi mbalimbali zinazoangazia utetezi wa jinsia mbalimbali zilizotengwa katika jamii. Kazi hii vilevile inatusaidia katika kuangazia na kuweka wazi namna ambavyo waandishi wa kike na wa kiume wanavyochangia katika kushughulikia masuala ya ukandamizaji wa jinsia mbalimbali na mambo yanayohusu jamii tunamoishi. Isitoshe, utafiti huu unachangia katika kutoa suluhu ya namna mbalimbali za kushughulikia suala la kukandamizwa kwa jinsia mbalimbali.

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biographies

Jackline Njeri Murimi

Chuo Kikuu cha Tom Mboya

Maingi Nkoroi Nancy

Chuo Kikuu cha Mount Kenya

References

Marejeleo
Anfred, M. (2004). Culture and Social Norms. New York: Dove Publishers.
Ayis, O. E. (1979). An Introduction to the African Culture 2nd ed. Nairobi: East African Educational Publishers.
Barbara, E. (1993). Let’s Discuss Women’s Right. England: Wayland Publishers.
Carol, J. O. (1986). Is There a Female Voice? Joyce Carol Oates Replies In ‘Feminist Literary Theory: A Reader’. Cambridge: Basil Blackwell Ltd. Uk. 208.
Carter, D. (2006). Literary Theory. Harpenden: Pockets Essentials.
Coats, M. (1994). Women’s Education: Society of Research in Higher Education and Open University Press.
Chesaina, C. (1987). Women in African Drama: Representation and Role: West Yorkshine: University of Leeds Press.
de’ Beauvoir, S. (1949). The Second Sex. London: Pan Books Publisher.
Eagleton, M. (1986). Feminist Literary Theory: A Reader. Malden: Blackwell Publishing.
Ellman, M. (1970). Thinking About Women. New York: Thomson Learning.
Habwe, J. (2007). Maisha Kitendawili. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Isiaho, J. K. (2001). “Taswira ya Mwanamke Katika Riwaya za Said Ahmed Mohamed” Tasnifu ya M. Phil. Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret. Haijachapishwa.
Jacobus, M. (1986). The Difference of View: Women Writing and Writing About Women in ‘Feminist Literary Theory: A Reader’. Uk. 216 – 219. Cambridge: Basil Blackwell Ltd.
Kimani, C. W. (2003). “Swala la Dhuluma Dhidi ya Wanawake Katika Fasihi ya Kiswahili.” Kohen, K. J. (1993). Women in Society. New York, London and Routledge: Marshall Cavendish.
Tasnifu ya Uzamili: Chuo Kikuu cha Kenyatta. Haijachapishwa.
Kobia, J. M. (2004). “Taswira za Mwanamke Katika Njuno za Katama G. C. Mkangi.” Tasnifu ya M. Phil Thesis. Chuo Kikuu cha Moi.
Matei, A. K. (2017). Chozi la Heri. Nairobi: One Planet Publishing & Media Services Limited.
Millet, K. (1970). Sexual Politics. Garden City, New York: Doubleday OCLC 489817513.
Momanyi, C. (1998). “Usawiri wa Mwanamke Katika Jamii ya Waswahili Kama Inavyobainika Katika Ushairi wa Kiswahili.” Tasnifu ya Uzamifu: Chuo Kikuu cha Kenyatta. Haijachapishwa.
___________ (2006). Tumaini. Nairobi: Longhorn Publishers.
___________ (2009). Nakuruto. Nairobi: Longhorn Publishers.
Published
2024-03-08
How to Cite
Jackline Njeri Murimi, & Maingi Nkoroi Nancy. (2024). USAWIRI WA WAANDISHI WA JINSIA TOFAUTI WANAVYOANGAZIA UKANDAMIZAJI WA KIJAMII KATIKA RIWAYA ZA MAISHA KITENDAWILI NA CHOZI LA HERI: AINA MBALIMBALI ZA UKANDAMIZAJI WA KINJINSIA KWA MUJIBU WA CHOZI LA HERI NA MAISHA KITENDAWILI. IJRDO- Journal of Educational Research, 10(1), 1-11. https://doi.org/10.53555/er.v10i1.6007